• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
SUMBAWANGA MUNICIPAL COUNCIL
SUMBAWANGA MUNICIPAL COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Manispaa
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi & Mipango Miji
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mazingira na Taka Ngumu
      • Mipango na Uchumi
      • Utawala & Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Matumizi bora ya Ardhi
    • Miundombinu yetu
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
    • Rasilimali za mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Huduma ya Maji
    • Education
    • Kilimo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati na majukumu yake
      • Fedha na Utawala
      • UKIMWI
      • Uchumi, Elimu & Afya
      • Mipango miji & Mazingira
    • Ratiba za Vikao
      • For Councilors
      • For Hon. Mayor
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
    • Huduma za Kisheria
    • Fedha
  • Kituo cha Habari
    • Albamu ya Picha
    • Video
    • Taarifa Kwa Umma
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Makala
    • Michezo & Burudani

MBUNGE AESH AIOMBA SERIKALI SASA KUFIKIRIA MIKAKATI YA UJENZI WA VYOO SHULENI

Ilibandikwa: November 25th, 2021

Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aesh Hilaly ameiomba serikali kufikiria kuongeza kiasi cha fedha za ujenzi wa vyoo vya wanafunzi baada ya zile ambazo zimetolewa kwaajili ya ujenzi wa vyumba madarasa ili kukamilisha dozi kamili ya kazi hiyo kubwa iliyofanyika.

Aesh ambaye anaendelea kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye Manispaa ya Sumbawanga licha ya kumshukuru Rais Samia Suluhu kwa kutoa fedha hizo za ujenzi wa vyumba vya madarasa alisema kuwa katika ukaguzi wake amebaini kuwa shule nyingi zina changamoto ya vyoo ambavyo vinatokana na wingi wa wanafunzi.

Alisema kila shule aliyopita amekutana na maombi ya Walimu na wanafunzi ambao licha ya kushukuru kwa ujenzi wa madarasa hayo lakini kilio chao ni matundu ya vyoo.

Mbunge huyo wa Sumbawanga Mjini alisema ipo haja ya kuiomba serikali kulizingatia jambo hilo kutokana na hali hiyo ambayo inatishia usalama wa afya za wanafunzi na Walimu wao.

Akizungumzia ujenzi wa madarasa hayo Aesh alimshukuru Rais Samia kwa kubaini changamoto hiyo hususan katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wa kidato cha Kwanza wanatarajia kujiunga na masomo yao mapema mwakani.

“Miaka mingine miezi kama hii tungelikuwa tumeshapokea maagizo kutoka Wizara ya TAMISEMI ambayo inatutaka wananchi na Watendaji wa halmashauri zetu kuhakikisha tunaongeza vyumba vya madarasa ili kuweza kuchukua wanafunzi wa kidato cha Kwanza kwenye shule zetu, lakini safari hii Mh.Rais ametusaidia sana kwa kutoa hizi fedha ambazo kila halmashauri inakimbizana kujenga madarasa yake”.alisema Aesh

Hatahivyo Aesh aliwaagiza Wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha wanajenga madarasa yenye viwango ili yaweze kudumu kwa miaka mingi huku wanafunzi wakiwa na uhakika wa masomo.

Aliwataka Wakuu wa shule hizo kujenga kwa kuzingatia bajeti na huku akiwataka kujiongeza zaidi ili fedha kidogo zitakazobaki zitumike kufanya vitu vingine vya maendeleo.

Manispaa ya Sumbawanga kwa mujibu wa Mkurugebzi wake Jacob Mtalitinya imepokea kiasi cha Shilingi Milioni 800.9, huku ikitakiwa kujenga vyumba vya madarasa 49, vine kati ya hivyo ni vya shule Shikizi.

Katika ziara hiyo Aesh ametoa mifuko Miamoja ya saruji kusaidi ujenzi wa vyoo kwenye Shukle ya Sekondari Sumbawanga ambacho ujenzi wake ulisimama kwa muda mrefu kutokana na mradi wake kuishiwa fedha, sanjari na choo cha wasichana kwenye Shule ya Sekondari Lukangao ambacho kilibomoka kwa muda mrefu, huku pia akisaidia mradi wa kupeleka maji kwenye Shule ya Sekondari Mhama ambayo ilikuwa haina maji.

Matangazo

  • Waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 December 18, 2020
  • Walichaguliwa Kidato cha Kwanza 2021 -PDF December 18, 2020
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU YA AWALI NA MSINGI TANZANIA BARA,JANUARY 2022. February 15, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 HALMASHAURI YA MANISPAA SUMBAWANGA. December 07, 2019
  • Angalia zote

Habari za Karibuni

  • MKURUGENZI MTALITINYA AZITAKA IDARA NA VITENGO VYATAKIWA KUFANYA MAFUNZO YA NDANI

    May 27, 2022
  • WAFANYABIASHARA RUKWA WATAKIWA KUFUATA SHERIA

    May 19, 2022
  • HOSPITALI YA WILAYA YA MANISPAA YA SUMBAWANGA YAANZA KUTOA HUDUMA

    May 05, 2022
  • KUKAMILIKA KWA UJENZI VYA VITUO VYA AFYA KWAONGEZA UHABA WA WATUMISHI H/MANISPAA YA SUMBAWANGA

    April 11, 2022
  • Angalia zote

Video

MANISPAA YA SUMBAWANGA KUTAFUTA MZABUNI WA KUZOA TAKA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • History
  • Councilors
  • Photo Gallery

Viunganishi vinavyofanana

  • Public Servant portal
  • Download your Salaryslip here
  • Looking for a job in Public Sector?
  • Get everything from the government
  • Rukwa
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Sumbawanga Municipal Council

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga

    Simu ya Mezani: +255252802163

    Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255

    Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Uhuru binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa