MRADI WA UPIMAJI NA UUZAJI WA VIWANJA 2000 ENEO LA NAMBOGO NA KATUMBA AZIMIO
UTANGULIZI:
Mradi wa upimaji viwanja Nambogo na Katumba Azimio umetekelezwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), hii itasaidia upatikanaji wa viwanja vilivyopimwa na kuwekewa miundombinu ya msingi na kusogeza huduma mbalimbali kwa wananchi waishio katika kata za pembezoni za Pito, Molo, Milanzi, Lwiche nk.
Utekelezaji wa mradi huu utasaidia kupunguza ujenzi holela, unaosababishwa na ongezeko la watu. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ilikuwa na watu 209,793 sawa na ongezeko la asilimia 43 % ya idadi wa watu 146,842 katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002.
Ongezeko hili la watu limesababisha ujenzi holela na usio na huduma za kijamii na kiuchumi kwa sababu miji mingi haikujiandaa kupokea idadi hiyo kubwa kwa ajili ya kuwapatia makazi na huduma zingine.
Aidha tafiti nyingi zinaonesha ukuaji huu wa kasi wa miji hauendi sambamba na upatikanaji wa huduma za kijamii na kiuchumi kama shule huduma za afya, maji, barabara, umeme miundombinu ya uzoaji taka n.k.
Jitihada mbalimbali zimeanza kuchukuliwa na Halmashauri kuweza kukabiliana na suala la upatikanaji wa viwanja vilivyopimwa kwa kutafuta wabia kutoka taasisi za umma na binafsi na pia kuzungumza na wamiliki wa ardhi kuingia makubaliano ya kupima viwanja na kisha kugawana asilimia ya viwanja vitavyozalishwa.
LENGO LA MRADI
Lengo kuu la mradi huu wa Nambogo ni kuwa na mji wa kisasa utakaokuwa na huduma mbalimbali ili kupunguza msongamano wa kufuata huduma katika eneo la kitovu cha mji (Central Business District) kwa siku za usoni. Sambamba na hilo, mradi utasaidia kuongeza upatikanaji wa viwanja vilivyopimwa na kuwekewa miundo mbinu ya msingi, hivyo kupunguza kasi ya ujenzi holela.
GHARAMA YA MRADI
Gharama za mradi zilizotumika Tshs. 1,589,692,000, ambazo kati ya hizo kiasi cha Tshs. 1,536,305,000, kimetolewa na GEPF na kiasi cha Tshs. 53,387,000 kimetolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Aidha Manispaa imetoa usimamizi wa kila siku wa mradi, wataalamu na ofisi kwa ajili ya uendeshaji wa mradi.
Uthamini na malipo ya fidia kwa wananchi 155 wenye ardhi umeshafanyika na kupewa stahiki zao kwa kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga```
FAIDA YA MRADI
Jedwali: viwango vya matumizi ya viwanja.
Na
|
Aina ya matumizi
|
Gharama kwa kila mita ya mraba
|
1
|
Makazi pekee (ujazo wa juu, kati na chini
|
2,700/= |
2
|
Makazi na biashara
|
3,000/= |
3
|
Biashara
|
5,000/= |
4
|
Huduma za jamii
|
3,500/= |
5
|
Ibada/ kuabudu
|
3,500/= |
6
|
Hoteli, vituo vya mafuta na maduka ya kuiwekezaji
|
5,000/= |
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo(aliyeshika ramani kushoto shati nyeusi na weupe) alipokwenda kutembelea Mradi wa Nambogo kujua maendeleo ya mradi huo akioneshwa namna mji huo utakavyokuwa kwenye ramani na afisa mipango miji wa Manispaa ya Sumbawanga Colman.
Eneo la Nambogo ndani ya Manispaa ya Sumbawanga lililopimwa viwanja kwaaajili na makazi na uwekezaji mbalimbali wa huduma za kijamii
ENEO LA VIWANDA NA MAGHALA “KANONDO INDUSTRIAL AREA”
Kanondo ni eneo ambalo limetengwa kwa matumizi ya viwanda vidogo. Eneo hili lina ukubwa mita za mraba 773,039 lipo kando ya barabara ya kwenda Mpanda.
Katika eneo hili lipo maeneo ambayo hayatauzwa ni pamoja na barabara, maeneo ya matumizi ya umma na viwanja 9 ambavyo vilitumika katika kuchangia gharama ya mchoro ili kuidhinishwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi.
Ukubwa wa eneo litakalouzwa
Eneo litakalouzwa litakuwa na mita za mraba 553,422.00 sawa na ekari 136.7 lenye viwanja 153
Bei elekezi ya viwanja ilitolewa na Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Kanda ya Kusini Magharibi tarehe 01/11/2016 kuwa ni Tsh. 3000/= kwa mita moja ya mraba (M2).
MPANGO KABAMBE (MASTER PLAN) 2015 – 2035 WA MIPANGO MIJI
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ilikuwa na Mpango Kabambe wa Miaka 20 kuanzia mwaka 1989 – 2009. Mwaka 2010 ulianza mchakato wa kuandaa mpango Kabambe wa miaka 20. Mchakato huo ulianza kwa hatua za awali mwaka 2011 za kuandaa Mpango Kabambe wa miaka 20 kama zinavyoainishwa kwenye sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya mwaka 2007 kifungu cha 8 eneo la Mipango miji lilitagazwa kwenye gazeti la Serikali Na. 223 ya tarehe 05/8/2011.
Hatua iliyofikiwa kwenye maandalizi ya Mpango Kabambe ni kukamilisha uandaaji wa taarifa (Rasimu) ya mwisho ya Mpango Kabambe ya kuwasilisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa ili aupitishe uwasillishwe kwa Mkurugenzi wa Mipango Miji wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Aidha kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2018.
Ombi kwa Wawekezaji
Wahi nafasi za kuwekeza katika Manispaa ya Sumbawanga, Mji ambao umepania kujipanga kisasa na kuleta mvuto wa miji inayoendelea kukua nchini, Manispaa ya Sumbawanga ndio makao makuu ya Mkoa wa Rukwa ambapo inaunganisha Mkoa wa Katavi na Songwe huku ikipakana na nchi ya Zambia na Congo kwa Upande wa Ziwa Tanganyika.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: 0784519681
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa